Home Uncategorized AZAM FC YAANZA KUIWINDA SIMBA, YAPANIA KUFANYA MAAJABU

AZAM FC YAANZA KUIWINDA SIMBA, YAPANIA KUFANYA MAAJABU


AZAM FC tayari wameanza maandalizi ya kuiwinda Simba kwenye mchezo wa ngao ya jamii utakaochezwa Agosti 17 uwanja wa Taifa.

Mchezo huo maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 23 utachezwa majira ya saa 1:00 usiku.

Jaffary Maganga, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ushindani mbele ya Simba.


Mchezo wa ngao ya jamii huwakutanisha mabingwa wa msimu, ambapo Simba ni kwa upande wa Ligi Kuu Bara huku Azam FC wakiwa ni mabingwa wa kombe la Shirikisho.

Msimu uliopita Simba ilitwaa ngao hiyo mbele ya Mtibwa Sugar kwa ushindi wa mabao 2-1.

SOMA NA HII  BREAKING: AZAM FC YASHUSHA JEMBE JINGINE LA KAZI