Home Habari za michezo BAADA YA KUICHEULIA TFF KUWA KOCHA WA STARS….NABI AFUNGUKA HAYA KUHUSU KOCHA...

BAADA YA KUICHEULIA TFF KUWA KOCHA WA STARS….NABI AFUNGUKA HAYA KUHUSU KOCHA MPYA…

Taifa Stars

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza kocha Mbelgiji Adel Amrouche kuwa kocha mpya wa kikosi cha Taifa Stars na uamuzi huo ukamuibua kocha wa Yanga Nasreddine Nabi akisema jamaa ni bonge la kocha.

Amrouche ametua Stars kuchukua nafasi ya Mdenishi Kim Poulsen aliondolewa Agosti mwaka jana baada ya timu hiyo kupoteza mechi nyumbani mbele ya Uganda katika mbio za fainali za CHAN zilizofanyika mwaka huu nchini Algeria.

Nabi mwenye uraia wa Ubelgiji kama Amrouche japo ana asili ya Tunisia, alisema kocha huyo mpya wa Stars ni rafiki yake wa muda mrefu ambapo urafiki wao ulitokana na falsafa za kocha huyo.

Nabi alisema Amrouche ambaye ana asili ya Algeria ni kocha mkubwa mwenye mafanikio na kwamba kama atapewa ushirikiano wa kutosha kwa wadau mbalimbali katika majukumu yake atairudisha timu hiyo kwenye ubora mkubwa.

“Najuana na Amrouche kwa miaka mingi ni rafiki yangu sana nadhani Mungu amewapa Watanzania kocha bora sana ambaye atawapa mafanikio makubwa,” alisema Nabi.

“Napenda sana falsafa zake ni kocha anayetamani kushinda zaidi mataji lakini ana mbinu nyingi nadhani Tanzania itarudi kwenye ramani nzuri ya soka la kuwa na timu imara kama atapewa ushirikiano mkubwa.

“Watu wa hapa wanapenda sana soka na timu zao nadhani Sasa hata kama wachezaji wanatakiwa kujitambua kwa kujiweka katika utayari wa kucheza soka la mafanikio kwa kujituma na nidhamu ya juu ili kazi ya kocha iwe rahisi.

“Siku zote hakuna kocha atatamani kutompa nafasi mchezaji mwenye kipaji na anayeonyesha juhudi mazoezini na uwanjani namtakia kila la kheri Adel (Amrouche).”

SOMA NA HII  SIMBA WAPANGUA KIKOSI CHA YANGA...NABI APANGA 'KUJILIPUA' DHIDI YA BIASHARA UNITED ILI AMUUE MNYAMA....