Home Habari za michezo SIMBA WAPANGUA KIKOSI CHA YANGA…NABI APANGA ‘KUJILIPUA’ DHIDI YA BIASHARA UNITED ILI...

SIMBA WAPANGUA KIKOSI CHA YANGA…NABI APANGA ‘KUJILIPUA’ DHIDI YA BIASHARA UNITED ILI AMUUE MNYAMA….


ILI kuhakikisha wanafikia malengo yao msimu huu, Kocha Mkuu wa Yanga, Nesreddine Nabi amepanga kupumzisha baadhi ya nyota wake wa kikosi cha kwanza katika mechi dhidi ya Biashara United kwa ajili ya kuwaweka fiti kuelekea mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Simba utakaochezwa Mei 28, mwaka huu.

Yanga itakutana na Biashara United kesho ikiwa ni siku tano zimebakia kabla ya kuvaana na Simba kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Nabi alisema anahitaji kuwapa mapumziko baadhi ya wachezaji wake kwa ajili ya kuwaandaa kisaikolojia na mchezo huo ambao hawahitaji kupoteza.

Nabi alisema uamuzi wa kufanya mabadiliko katika mchezo dhidi ya Biashara United unalenga kuongeza nguvu ya kuwakabili Simba na hatimaye kusonga mbele kwenye michuano hiyo ambayo watani zao pia wanaushikilia ubingwa.

“Ni mechi ngumu na yenye presha kubwa kwa sababu tayari tumekuwa na asilimia kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi lakini pia bado tunahitaji taji la Kombe la FA, lazima tushinde dhidi ya Simba ili tucheze fainali,” alisema Nabi.

Aliongeza wanahitaji kutafuta matokeo mazuri katika michezo yote ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyobakia pamoja na kushinda mechi dhidi ya Simba na ili wafikie malengo, analazimika kupangua kikosi chake.

“Huu wakati nalazimika kuwatumia wachezaji wote waliopo ndani ya kikosi changu na kwa wale walitumika sana wanahitaji kupumzika,” Nabi alifafanua.

Alisema bado wachezaji wake wanatakiwa kupambana katika kila mechi wanayocheza kwa sababu bado hawajamaliza kazi na hawajafikia malengo waliyonayo ya msimu huu unaoelekea ukingoni.

SOMA NA HII  DODOMA JIJI KAMA SIMBA NA YANGA TU...NAO WAAMUA KUONYESHA UBABE KWA HILI...