Home Habari za michezo DODOMA JIJI KAMA SIMBA NA YANGA TU…NAO WAAMUA KUONYESHA UBABE KWA HILI…

DODOMA JIJI KAMA SIMBA NA YANGA TU…NAO WAAMUA KUONYESHA UBABE KWA HILI…

Mabosi wa Dodoma Jiji wameamua kufanya kweli kwa msimu ujao, baada ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa KMKM ya Zanzibar, Yassin Mgaza.

Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kuanzia msimu ujao.

Mgaza ndiye kinara wa mabao wa Ligi Kuu Zanzibar akiwa amefungwa mara 17 na pasi nane za mabao katika mechi 25 alizocheza, huku ukiwa ni msimu wake wa kwanza katika ligi hiyo.

Mtu wa karibu na mchezaji huyo kutoka Zanzibar aliliambia Mwananchi kuwa mchezaji huyo bado alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja, lakini makubaliano yameshafanyika na KMKM itamuachia kwa ajili ya kujiunga na Dodoma Jiji.

“Alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja ila kila kitu kimefanyika na muda wowote atatangazwa kujiunga na Dodoma Jiji, kwani tayari ameshamalizana nao.

“Dodoma Jiji ilikuwa inamfuatilia Yasin tangu akiwa na Mbuni FC (Championship), kwa sababu kule napo alikuwa anafanya vizuri, hata kuja huku ni sehemu tu ya wao kuendelea kumuangalia na ndiyo maana imekuwa ni rahisi usajili wake kukamilika,” kilisema chanzo hicho.

Mgaza, ambaye ni msimu wake wa kwanza KMKM akitokea Mbuni FC, aliisaidia timu yake ya zamani (Mbuni FC) kupanda daraja akihusika kwenye mabao 22 kwa kufunga 16 na kutoa asisti sita kwenye mechi 16.

SOMA NA HII  NDAYIRAGIJE KOCHA MKUU GEITA GOLD