Home Burudani TEMEKE KOMBAINI YABEBA KOMBE LA Infinix HOT LEAGUE KIBABE….KILA MCHEZAJI KAPEWA SIMU...

TEMEKE KOMBAINI YABEBA KOMBE LA Infinix HOT LEAGUE KIBABE….KILA MCHEZAJI KAPEWA SIMU MPYA KALIII YA HOT 12…


Ule mtanange wa kukata na shoka kati ya TEMEKE KOMBAINI chini ya Yusuphu Mkule  dhidi ya KINONDONI KOMBAINI ya George Job, ulipigwa jioni ya jana  katika Dimba la Kinesi, ikiwa ndio fainali ya mashindano hayo.

TEMEKE imeweza kushinda kwa mikwaju ya penati 4- 2 baada ya timu zote mbili kutoka suluhu ya bila kufungana ndani ya dakika 90. 

Kinondoni ilitinga fainali baada ya kuwatoa timu ya chuo cha ustawi wa jamii wakati Temeke wakiwa toa Ardhi katika hatua ya nusu fainali.


Fainali hiyo TEMEKE wamejishindia simu aina ya HOT 12 kwa kila mchezaji, set ya jezi  pamoja fedha  taslim, wakati kinondoni wakipata Infinix HOT 11 kwa kila mchezaji na set ya jezi pia. 

Nafasi ya Mshindi wa tatu ilikuchukuliwa na chuo cha Ustawi wa jamii baada ya kuwafunga chuo cha  Ardhi kwa goli 4-2, hivyo kuwafanya ustawi kujichukulia simu mpya za infinix HOT 11PLAY kwa kila mchezaji pamoja na set ya jezi.


Msimu wa kwanza mashindano ya HOT League yenye lengo ya kuwapa vijana waliopo vyuoni na wale waliopo wilaya mbalimbali kukutana na kuonesha vipaji vyao yamefikia tamati kwa msimu wa kwa nza, huku Infinix wakitoa ahadi ya kuyaleta tena kwa msimu mwingine kwa ukubwa zaidi. 

Inifnix HOT League ililetwa udhamini wa SIMU mpya ya  HOT 12,  toka infinix yenye 

*Betri kubwa 6000, GB 128 , *Processor ya Helio G85 yenye uwezo wa kuchaji kwa haraka zaidi watt 18. (Fast charge)

#HOT12SeriesFastnFun  #InfinixHOTLeague

SOMA NA HII  MASTAA YANGA WAANZA KUMCHANGANYA GAMONDI MAPEMAAAA