Home Habari za michezo PAMOJA NA KIPOGO CHA JANA…SIMBA WAPELEKA AKILI UGANDA NA GUINEA…

PAMOJA NA KIPOGO CHA JANA…SIMBA WAPELEKA AKILI UGANDA NA GUINEA…

Habari za Simba

Baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo za Kundi C katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC sasa imepanga kufa na Vipers na Horoya katika mechi zijazo za hatua hiyo.

Simba ambayo jana ilicheza nyumbani Uwanja wa Mkapa, Dar dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco, ilikubali kichapo cha mabao 0-3.

Wageni Raja Casablanca walipata mabao yao kupitia Hamza Khabba (dk 30), Soufiane Benjdida (dk 82) na Ismael Mokadem (dk 86) kwa penalti.

Kipigo hicho kimeifanya Simba kuburuza mkia wa Kundi C ikiwa haina pointi baada ya kupoteza mechi mbili dhidi ya Horoya (1-0) na Raja Casablanca (0-3).

Mechi mbili zijazo, Simba itacheza dhidi ya Vipers, ikianzia ugenini Februari 25, kisha nyumbani Machi 7, baada ya hapo, itakuwa nyumbani tena dhidi ya Horoya kati ya Machi 17 na 18, kabla ya kumalizana na Raja Casablanca ugenini kati ya Machi 31 na Aprili Mosi.

Simba imeapa katika mechi tatu zijazo dhidi ya Vipers na Horoya, itakufa na wapinzani wao hao kuhakikisha inakusanya pointi zote tisa kufufua matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali.

Katika Kundi C, vinara ni Raja Casablanca wenye pointi sita wakishinda mechi zote mbili za kwanza, wakifuatiwa na Horoya wenye nne, huku Vipers wakikamata nafasi ya tatu wakiwa na pointi moja waliyoipata jana katika suluhu nyumbani dhidi ya Horoya.

Simba katika mechi mbili ilizocheza, imeruhusu mabao manne, huku ikiwa haijafunga hata moja ambapo jana ilishuhudiwa dakika tisini ikipiga mashuti 11, kati ya hayo, matatu yalilenga lango. Wapinzani wao walipiga mashuti 11, sita yakilenga lango na matatu yakijaa wavuni.

SOMA NA HII  BAADA YA KISINDA KURUHUSIWA KUCHEZA LIGI KUU...JEMEDARI SAIDI AIBUKA NA KUTUPA KOMBORA HILI KWA TFF..