Home Habari za michezo BAADA YA KIPIGO CHA JANA…MBRAZILI AJITETEA SIMBA…ADAI HAKUPATA MUDA WA KUANDAA TIMU…

BAADA YA KIPIGO CHA JANA…MBRAZILI AJITETEA SIMBA…ADAI HAKUPATA MUDA WA KUANDAA TIMU…

Habari za Simba SC

Baada ya Simba kupoteza kwa magolo 3-0 dhidi ya Raja Casablanca, Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira Robertinho amesema wakati anajiunga na timu hiyo hakupata muda mzuri wa kufanya maandalizi jambo ambalo limesababisha kutokufanya vizuri katika michuano ya Kimataifa tangu akabidhiwe kikosi.

“Nafikiri timu yangu imecheza vizuri lakini ilitakiw akucheza kwa umakini zaidi ya ilivyokuwa, ndivyo mchezo wa soka ulivyo, Raja wamekuwa wazuri kuliko sisi.

“Tunatakiwa kusahau kuhusu mchezo huu na kuelekeza mawazo yetu katika mchezo ujao. Nilipoteza wachezaji kadhaa kutokana na kuwa majeruhi kama Saido na Baleke ambao wote walihtaji kuwa na utayari mzuri kabla ya mchezo wa leo.

“Nilipokuja hapa sikupata muda wa kuiandaa timu mwanzoni mwa msimu, nimekutana na mazingira ya mechi mechi baada ya mechi, nahitaji muda wa kuwaandaa kifiziki na kimbinu.

“Kipindi cha pili tulicheza vizuri lakini hatukucheza kwenye malengo sahihi. Tulipata nafasi kadhaa hatukutumia vizuri, wenzetu wamepata nafasi wametumia vizuri, sasa tuangalie mchezo unaofuata dhidi ya Vipers,” amesema Robertinho.

SOMA NA HII  SIMBA YAANDAMWA NA NJAA KALI...KOCHA MKUU ATHIBITISHA...AMEZUNGUMZA HAYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here