Home Uncategorized YANGA YATOA TAMKO KUHUSU KUJIUZULU KWA VIONGOZI WAO PAMOJA NA WALE WALIOJIENGUA

YANGA YATOA TAMKO KUHUSU KUJIUZULU KWA VIONGOZI WAO PAMOJA NA WALE WALIOJIENGUA


HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kilichotokea kwa baadhi ya viongozi wa Kamati ya Utendaji ndani ya Yanga kujiuzulu na wengine kuenguliwa madarakani ni mtikisiko kwa muda ila kila kitu kitakuwa sawa.

Machi 27 viongozi watatu ndani ya Yanga walijiuzulu huku wawili wakiondolewa kwenye madaraka yao na Kamati ya Nidhimamu ya Yanga.

Waliosimamishwa na Kamati ya Utendaji ya Yanga iliyochukua hatua ya kinidhamu ni Salim Rupia na Frank Kamugisha Machi 27 na wajumbe watatu ambao ni Rogers Gumbo, Shija Richard na Said Kambi wamejiuzulu.


Bumbuli amesema :” Ni mtikisiko lakini ni kawaida kwa timu ya Wananchi kutokea kila kitu kitakuwa sawa na mipango inaendelea,” .

SOMA NA HII  MOHAMMED DEWJI 'MO; AJA NA TAMKO ZITO KUHUSIANA NA SIMBA