Home Uncategorized MTUPIAJI NONGA AINGIA ANGA ZA YANGA

MTUPIAJI NONGA AINGIA ANGA ZA YANGA

PAUL Nonga, nahodha wa Klabu ya Lipuli inaelezwa kuwa yupo kwenye rada za mabosi wake wa zamani Yanga ambao wanataka kurejesha saini yake.

Nonga aliwahi kukipiga ndani ya Yanga enzi za Hans Pluijm aliomba kusepa ndani ya kikosi hicho baada ya kukosa namba kikosi cha kwanza ila kwa sasa amekuwa bora ndani ya Lipuli.

Msimu huu Nonga amevunja rekodi yake ya mabao ya msimu uliopita 2018/19 ambapo alifunga mabao matano huku msimu huu wa 2019/20 akitupia mabao 11 jambo linalowapa matumaini Yanga kuiwinda saini yake. 

 Nonga amesema kuwa ana dili nyingi mkononi ila hawezi kutaja kwa sasa atasaini wapi kwani tayari ameshawaaga mabosi zake Lipuli. “Nimeshawaaga mabosi zangu Lipuli ili watafute mbadala mwingine ila nitakapoibukia nitajua mwenyewe wakati ukifika,” amesema Nonga.

SOMA NA HII  PIALALI NA TINAMPAY TAMBO TUPU MWANZO MWISHO KABLA YA VITASA