Home Habari za michezo SAIDO NTIBAZONKIZA AVUTA ‘KICHUNA’ BURUNDI…KUHUSU HATMA YAKE NA KURUDI YANGA..ISHU IKO HIVI..

SAIDO NTIBAZONKIZA AVUTA ‘KICHUNA’ BURUNDI…KUHUSU HATMA YAKE NA KURUDI YANGA..ISHU IKO HIVI..


MSHAMBULIAJI wa Yanga  Mrundi Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ juzi amefunga ndoa na mpenzi wake Samatha Uwera (Samira) Bujumbura Burundi na sherehe kufayika kwenye ukumbi wa Beliane na anatarajiwa kutua nchini kabla ya mechi na Azam, April 6, Mwaka huu.

Wakati Saido akifurahia ndoa hiyo, chama lake Yanga lilikuwa uwanjani ikicheza mechi ya ligi dhidi ya KMC na kushinda 2-1 kwa bao la Andrew Vicent aliyejifunga na lile la pili likipachikwa kwa kichwa na Djuma Shaban.

Hata hivyo Saido hakuonekana uwanjani kwenye mechi mbili za Yanga zilizopita kutokana na kuuguza jeraha la mguu alilolipata kwenye mechi ya ligi dhidi ya Kagera Sugar chama lake likishinda 3-0, huku akitupia bao la tatu la mchezo huo.

Na inafahamika kuwa Saido anaendelea vizuri na  atarejea nchini mwishoni mwa mwezi huu na moja kwa moja atajiuga na timu kuendelea kujifua kwaajili ya mechi zijazo ikiwemo dhidi ya Azam inayotarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake.

Saido msimu huu amekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga akihusika katika mabao 11 ya timu hiyo akifunga sita na kuasisti tano.

SOMA NA HII  NTIBANZOKIZA ATAJWA KUZINGUANA NA KOCHA YANGA