Home Uncategorized PIALALI NA TINAMPAY TAMBO TUPU MWANZO MWISHO KABLA YA VITASA

PIALALI NA TINAMPAY TAMBO TUPU MWANZO MWISHO KABLA YA VITASA


 KUELEKEA pambano kali la kimataifa la ngumi kati ya Bondia Mtanzania, Idd Pialali ‘Simba’ na Mfilipino Arnel Tinampay, mambo yamepamba moto, ambapo mabondia hao kila mmoja ametamba kuhakikisha anamkalisha mpinzani wake mapema tu kwenye pambano hilo litakalofanyika Novemba 28, mwaka huu kwenye ukumbi wa Next Door Arena jijini Dar es Salaam.

Pialali amesema: “Nawaomba mashabiki wa ngumi wajitokeze kwa wingi siku ya Jumamosi ili kuja kushuhudia burudani ya kutosha niliyowaandalia.

 

“Nataka niwahakikishie kuwa hapa hakuna ushindi wa pointi ni lazima mtu akae kwa KO mapema tu ili wasije wakatuzoea, hivyo nimejiandaa kumchakaza mapema huyu Mfilipino.”


Naye Tinampay akijibu tambo hizo alisema: “Natamani mashabiki wangu waanze kutangulia pale Next Door Arena leo hii kwa sababu kuna sapraizi ya burudani ya kutosha kwa ajili yao nimeiandaa.


“Najua Pialali ni bondia mzuri lakini tayari nimemsoma na haitakuwa ngumu kumpiga.”


Pambano hilo limedhaminiwa na Gazeti la Spoti Xtra, +255 Global Radio, DSTV, Plus TV, Precission Air, Smart Gin, Kebby’s Hotel na Uhuru FM ambapo pia siku hiyo litashuhudiwa pambano jingine la kimataifa kati ya bondia Mtanzania, Salim Mtango kutoka Tanga ambaye atapanda ulingoni kuzichapa na Eduardo Mancito wa Ufilipino.

SOMA NA HII  NYOTA CHELSEA AGOMEA DILI LA KUTUA JUVE KISA KUHOFIA KUSHUKA KIWANGO