Home Taifa Stars TANZANIA YATWAA UBINGWA WA CECAFA U 23, KOCHA AWAPA TANO

TANZANIA YATWAA UBINGWA WA CECAFA U 23, KOCHA AWAPA TANO

 KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, chini ya miaka 23 amesema kuwa amefurahishwa na vijana wake kuweza kutwaa taji la Cecafa 2021.


Ni kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Burundi ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa Uwanja wa Bahir Dar uliopo nchini Ethiopia.

Ushindi wa Tanzania umepatikana kwa penalti 6-5 dhidi ya Burundi baada ya dakika 90 ngoma kuwa nzito kwa timu zote mbili kupata ushindi.

Ni penalti ya mwisho ya kijana Rajab Athuman ambaye alipiga kiufundi ikazama mazima nyavuni baada ya ile ya Akizimana wa Burundi kugonga mwamba mbele ya kipa namba moja Metacha Mnata.

Mnata hakuwa na chaguo leo kwa kuwa penalti zote tano zilizama nyavuni licha ya dakika 90 kutimiza majukumu yake kwa kuokoa michomo mitatu mikali iliyopigwa na washambuliaji wa Burundi.

Poulsen amesema:”Ni furaha kwangu na vijana pamoja na taifa kiujumla kwa kupata matokeo mazuri ambayo tulikuwa tunahitaji.

“Ilibidi nifanye mabadiliko kwenye kikosi kwa sababu wachezaji walikuwa wamechoka kutokana na kucheza mechi nyingi za ushindani ila mwisho wa siku tumeshinda,” .

SOMA NA HII  KUELEKEA AFCON ....WAZIRI WA MICHEZO ATAJA WACHEZAJI WAKUTUMIKA TAIFA STARS....