Home Taifa Stars TANZANIA YATOSHANA NGUVU NA DR CONGO….MZAMIRU, FEI TOTO WAANDIKA REKODI

TANZANIA YATOSHANA NGUVU NA DR CONGO….MZAMIRU, FEI TOTO WAANDIKA REKODI


TIMU ya Taifa ya Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen leo Septemba 2 imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya DR Congo.

Mchezo wa leo ambao ulikuwa ni wa kufuzu Kombe la Dunia dk 45 za mwanzo ngoma ilikuwa 1-1 na ni DR Congo walianza kumtungua Aishi Manula.

Bao la Tanzania lilifungwa na Simon Msuva dk 36 kwa shuti kali ambalo lilimshinda mlinda mlango wa DR Congo na kumfanya asawazishe bao la Merci Mbokane aliyepachika dk 25.

Nyota Msuva alikwama kuyeyusha dk zote 90 kwa kuwa alipata maumivu dk 89 na nafasi yake ilichukuliwa na Abraham Meshack. 

Pia katika mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa TP Mazembe nyota wawili wa Tanzania walionyeshwa kadi za njano ikiwa ni pamoja na Mzamiru Yassin na Feisal Salum hawa wote ni viungo wa kati hivyo kuweka rekodi ya kuwa wachezaji wa kwanza wa Tanzania kuonyewshwa kadi kwenye michuano hio.

Mchezo ujao wa Tanzania iliyo kundi J ni dhidi ya Madagascar unatarajiwa kuchezwa Septemba 7, Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  KOCHA ZAMBIA ATOA KAULI YA KIBABE AKIIVAA TANZANIA