Home kimataifa MJUMBE HAZARD MAFANIKIO KAYAACHA CHELSEA

MJUMBE HAZARD MAFANIKIO KAYAACHA CHELSEA


ALIJIUNGA na Real Madrid inayoshiriki La Liga, Julai Mosi,2019 akitokea Klabu ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu England, anaitwa Eden Hazard na mkataba wake unatarajiwa kumeguka Juni 30,2024.
Umri wake ni miaka 30, alizaliwa Januari 7,1991 ni raia wa Ubelgiji, anaimudu vema nafasi ya kiungo mshambuliaji na alikabidhiwa jezi namba 7 iliyowahi kuvaliwa na Cristiano Ronaldo alipokuwa akivaa uzi wa Real Madrid.

Akiwa ndani ya Chelsea alicheza jumla ya mechi 245 ilikuwa kuanzia msimu wa 2012/2019 rekodi zinaonyesha kwamba alitupia mabao 85.

Hayo ni mafanikio makubwa kwa kiungo huyo akiwa katika timu moja inayoshiriki ndani ya Ligi Kuu England.

Akiwa ndani ya uzi wa Real Madrid amecheza jumla ya mechi 33 huku akiwa ametupia jumla ya mabao manne.Maisha yake yamekuwa tofauti na matarajio ya mashabiki wengi kwa kuwa amepoteza ule ufalme wake aliokuwa nao Chelsea.
 Ni amecheza timu tofauti ikiwa ni pamoja na Lille inayoshiriki Ligue 1 aliweza kutwaa mataji tofautitofauti yaliyomfanya aweze kuwa na furaha kwa wakati huo.

Lakini inaonekana kuwa mafanikio makubwa aliyapata zama akiwa ndani ya Chelsea kwa kuwa alinyanyua mataji mengi tofauti na timu nyingine alizopata kuzitumikia katika majukumu yake.

Msimu wa 2018/19 pamoja na ule wa 2012/13 aliweza kushinda taji la Europa League, msimu wa 2015 alishinda taji la English League Cup msimu wa 2018 alishinda taji la FA Cup, taji la Ligi Kuu England alitwaa mara mbili ilikuwa msimu wa 2017 na 2015 mataji haya yote ilikuwa ndani ya Klabu ya Chelsea.

Hivyo akiwa ndani ya Chelsea aliweza kushuhudia timu yake ikitwaa mataji mara sita katika mashindano tofautitofauti idadi ambayo ni kubwa kwake katika maisha ya soka.

Pia aliweza kutwaa taji la ubingwa wa Hispania, maarufu kama La Liga, mara moja msimu wa 2019/20 na taji la Hispania Super Cup mara moja msimu wa 2019/20 haya ilikuwa ndani ya Real Madrid na alitwaa mataji mawili akiwa ndani ya Lille ilikuwa msimu wa 2010/11.

Mjumbe Hazard hajawa mwenye furaha ndani ya Real Madrid kwa kuwa amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya enka ya mara kwa mara jambo ambalo linamfanya ajenge ushkaji na benchi.

Pia kusepa kwake ndani ya Chelsea kunamfanya aweze kuyaacha mafanikio yake mengi aliyokuwa anatabirwa hapo baadaye mpaka pale atakapojipanga tena kuweza kurudi kwenye ubora wake.
SOMA NA HII  ARSENAL: HATUKUSTAHILI KUFUNGWA