Home Habari za michezo KISA KUKATALIWA OMBI LAKE LA KUUZWA….RONALDO AGOMEA MAZOEZI MAN UTD….MABOSI ZAKE ‘WAMDINDIA...

KISA KUKATALIWA OMBI LAKE LA KUUZWA….RONALDO AGOMEA MAZOEZI MAN UTD….MABOSI ZAKE ‘WAMDINDIA KISELA’…


Nyota wa Manchester United, Cristiano Ronaldo, hajajiunga na wachezaji wenzake jana kwa ajili ya mazoezi baada ya mapumziko, kutokana na matatizo ya kifamilia.

Ronaldo mapema aliwaambia mabosi wa United kuwa anataka kuondoka dirisha hili, endapo ofa nzuri itawekwa mezani.

Hata hivyo timu hiyo imesisitiza Ronaldo hatauzwa, kwani yupo kwenye mipango ya kocha mpya aliyeteuliwa, Erik ten Hag.

Sasa kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Fabrizio Romano, Mreno huyo hakuungana na wenzake jana kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya, yalioanza tangu wiki iliyopita.

Staa huyo alikuwa mapumzikoni na familia yake, tangu alipomaliza mechi za makundi ya michuano ya Natione League, mwezi uliyopita.

Wachezaji wengine wa kikosi cha Man United walioripoti mazoezi jana ni Raphael Varane, Bruno Fernandes, Fred, Alex Telles, Anthony Elanga, na Scott McTominay.

SOMA NA HII  KISA CAF...NABI NA MGUNDA WAINGIA KWENYE MTIFUANO NA TFF...HOJA ZAO HIZI HAPA...