Home Habari za michezo KUHUSU LILE DILI LA LUIS MIQUISSONE KURUDI SIMBA …MAMBO YAKO NAMNA HII...

KUHUSU LILE DILI LA LUIS MIQUISSONE KURUDI SIMBA …MAMBO YAKO NAMNA HII KUMBE…KOCHA MPYA AL AHLY HAMTAKI….


Klabu ya Simba, ipo kwenye wakati mzuri wa kumrudisha kikosini hapo kiungo mshambuliaji raia wa Msumbiji, Luís Jose Miquissone kutoka Al Ahly ya Misri.

Hiyo ni baada ya Luis kuwa na wakati mgumu ndani ya Al Ahly tangu alipojiunga na timu hiyo Agosti 26, 2021 akisaini mkataba wa miaka minne akitokea Simba.

Baada ya Al Ahly kuachana na Kocha Mkuu, Pitso Mosimane na nafasi yake kuchukuliwa na Ricardo Soares, imeripotiwa kwamba Luis hana maisha tena kikosini hapo.

Kwa mujibu wa mabosi wa Al Ahly, kiungo huyo tangu ametua hapo, hajaonesha kiwango kizuri, hivyo Soares, baada ya kuangalia tathmini ya kikosi chake, amemuondoa Luis kwenye mipango yake. Kwa sasa Al Ahly inaangalia namna ya kusajili mchezaji mwingine wa nafasi yake.

Uamuzi uliochukuliwa ni kumuachia Luis aondoke kikosini hapo iwe kwa mkopo au kuuzwa moja kwa moja, kwa sasa anasubiriwa Miquissone na wawakilishi wake kujadili hilo kabla ya kufanyika uamuzi.

Wakati Luis anauzwa, uongozi wa Simba ulisema kwamba, walikubaliana na Al Ahly kwamba mchezaji huyo endapo akiondoka Al Ahly, Simba ina nafasi ya kwanza kumrudisha hapa nchini kuliko timu yoyote ya Tanzania.

SOMA NA HII  BAADA YA VIKAO VIIINGI...HATIMAYE CHAMA HUYU HAPA..WAMOROCO WAKUBALI YAISHE....