Home CAF RASMI….AFRICA SUPER LEAGUE KUANZA MWAKA 2023…TIMU 24 KUSHIRIKI…BINGWA KULAMBA BIL 23….SIMBA NAO...

RASMI….AFRICA SUPER LEAGUE KUANZA MWAKA 2023…TIMU 24 KUSHIRIKI…BINGWA KULAMBA BIL 23….SIMBA NAO WAMO…


Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF Patrice Motsepe amesema wanategemea kuanza kuandaa mashindano mapya ya klabu ambayo yatafahamika kama Super League kuanzia mwaka Agosti 2023.

Motsepe amesema hayo wakati akizungumza Jijini Rabat, Morroco ambapo walikuwa kwenye kikao cha shirikisho hilo kujadili masuala mbalimbali likiwemo la kubadilisha mwezi na mwaka wa fainali ya AFCON pamoja na kubadilisha utaratibu wa kuchezwa kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.

Raia huyo wa Afrika Kusini aliyechukua nafasi ya Ahmad raia wa Madagascar amesema kutokana na klabu nyingi kuwa na ukata wa fedha halafu makampuni mbalimbali kuonyesha nia ya kudhamini mashindano hayo wameona ni muhimu kuwa na michuano hiyo itakayoanza na timu 24 ambapo kwa Tanzania, Simba SC inatazamiwa kuiwakilisha kwenye mashindano hayo.

Timu hizo zitapatikana kulingana na nafasi zao kwenye viwango vya Fifa lakini bingwa wa mashindano atachukua kitita cha dola za kimarekani milioni 10 (23,280,000,000) wakati jumla mashindano hayo yatakuwa na dola za kimarekani milioni 100 (Tsh 232,800,000,000).

Pamoja na kuibuka kwa mashindano mengine, Motsepe amesema Ligi ya Mabingwa ambayo huusisha mataifa yote barani Afrika yataendelea kama kawaida.

Mpango wa Super League kwa bara la Ulaya uliishia njiani baada ya kudumu kwa takribani wiki moja ambapo klabu mbalimbali zilikubali kujiunga kabla ya kutoka ikiwemo zile kubwa kwenye Ligi tano bora.

SOMA NA HII  ZA NDAANII...HUU HAPA UKWELI KUHUSU STRAIKA MPYA WA YANGA KUTOFIKA NCHINI PAKA SASA...