Home Uncategorized JEMBE JIPYA SIMBA LAPANIA KUFANYA MAKUBWA NDANI

JEMBE JIPYA SIMBA LAPANIA KUFANYA MAKUBWA NDANI

CHARLES Ilanfya, straika mpya ndani ya Klabu ya Simba ambaye inaelezwa kuwa amesaini dili la kuitumikia klabu hiyo kwa msimu wa 2020/21, amepania kufanya makubwa ndani ya timu hiyo.
Ilanfya ambaye ataibukia Simba akitokea KMC, ametupia jumla ya mabao sita kati ya 35 ambayo yamefungwa na timu hiyo kwa msimu wa 2019/20.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ilanfya alisema kuwa iwapo dili lake la kuibukia ndani ya Simba litatimia, ataendeleza zaidi moto alionao.
“Suala langu kwa sasa nimemuachia meneja wangu yeye ndiye anayejua mpango mzima lakini ikitimia na nikawa ndani ya Simba basi nitafanya makubwa kwa kuwa ninaamini katika uwezo wangu.
“Nimefunga mabao sita ndani ya timu yangu ya KMC na nilikuwa nje kwa muda kwa sababu ya majeraha ila kwa sasa nipo fiti na ninaendelea vizuri, hivyo nitapiga kazi mwanzo mwisho,” alisema Ilanfya.
SOMA NA HII  GADIEL MICHAEL APANIA KUFANYA MAKUBWA NDANI YA SIMBA