Home news BAADA YA KUONA MAMBO MAZITO…NCHIMBI ATEMANA NA YANGA MAZIMA..UONGOZI WAFUNGUKA HAYA…

BAADA YA KUONA MAMBO MAZITO…NCHIMBI ATEMANA NA YANGA MAZIMA..UONGOZI WAFUNGUKA HAYA…


WAKATI kikosi cha Yanga kilikuwa visiwani Zanzibar kikiendelea na maandalizi ya Ligi, mshambuliaji wao Ditram Nchimbi amejiondoa mwenyewe kikosini.

Nchimbi alijiunga na Yanga Desemba 19 2019 ameitumikia timu hiyo miaka miwili baada ya kuona mambo yake sio mazuri ndani ya timu hiyo ameamua kujiengua mwenyewe.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa ni kweli mchezaji huyo hayupo pamoja na timu ni baada ya mkataba wake kumalizika na uongozi haujaonyesha nia ya kumuongeza mkataba.

β€œMkataba wake umeshakwisha na mchezaji mwingine ambaye mkataba wake upo ukingoni ni Adeyum Saleh yeye anamalizia msimu huu sijajua kama uongozi utakuwa na mpango naye,” alisema.

Alisema Ditram ameshaaga hatakuwa miongoni mwa wachezaji wa Yanga akizungumzia maandalizi yao kwa ujumla alisema wanaenda vizuri na mipango ya kocha imeenda kama ilivyopangwa. β€œKocha aliomba michezo miwili yote imechezwa wachezaji wote ameona mapungufu na uwezo wao hasa nyota ambao walikuwa nje kwa muda mrefu kama Yasin Mustafa amerudi na amepewa muda wa kucheza sasa ni yeye kuamua.”

SOMA NA HII  ZA NDANII KABISAA....PABLO CHANZO CHA MORRISON KUTEMWA SIMBA...ALIMFUKUZA MCHANA KWEUPEE...