Home Habari za michezo KUHUSU CHAMA NA KUONGEZA MKATABA SIMBA…UKWELI UNAOPASWA KUJUA HUU HAPA…

KUHUSU CHAMA NA KUONGEZA MKATABA SIMBA…UKWELI UNAOPASWA KUJUA HUU HAPA…

Habari za Simba SC

Meneja wa Habari na Mawasilino wa SImba SC Ahmed Ally amefichua kufikiwa kwa makubalino kati ya Uongozi wa Klabu hiyo na Kiungo kutoka Zambia Clatous Chota Chama.

Pande hizo mbili zilikuwa katika mazungumzo ya kusaini mkataba mpya, kufuatia mkataba wa awali wa kiungo huyo kutarajia kufikia kikomo mwezi Januari 2024.

Ahmed Ally amefichua siri hiyo kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii akieleza kuwa, Chama amekubali kusalia Simba SC, na atakaporejea nchini Tanzania atasaini mkataba mpya wa miaka miwili.

Chama alisaini mkataba na Simba SC mwezi Januari 2021 aliposajiliwa tena klabuni hapo akitokea RS Berkane ya Morocco, ambako alishindwa kucheza soka lake, kutokana na mazingira ambayo alidai hayakuwa rafiki kwake na familia yake.

Ahmed Ally ameandika: Chama amekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili zaidi kuendelea kuitumika Simba Sports Club

Mkataba utasainiwa akirejea Tanzania baada ya majukumu ya timu ya taifa na mapumziko kabla ya Pre Season.

SOMA NA HII  PATA BONASI MPAKA YA 80000/ KUTOKA MERIDIAN BET SASA

1 COMMENT

  1. Msitu anime wanachama Simba sport club Kwa kubania fedha za usajili, mpaka tunazidiwa na hao,,,,,,,,,,,,,,,,,, watumwa wa fikra

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here