Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA POLISI TZ…NABI AANZA VISINGIZIIO…AHOFIA KUTILIWA MCHANGA KWENYA KITUMBUA CHAKE…

KUELEKEA MECHI NA POLISI TZ…NABI AANZA VISINGIZIIO…AHOFIA KUTILIWA MCHANGA KWENYA KITUMBUA CHAKE…


Kocha wa Yanga, Mohammed Nabi amesema anatambua anatambua mechi yao dhidi ya Polisi Tanzania itakuwa ngumu lakini wamejiandaa kwa ajili ya kuondoka na alama tatu.

Nabi ameyasema hayo jana Agosti 15, 2022 alipokuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa ajili ya safari ya kwenda kuwavaa Polisi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

β€œTunafahamu Polisi wanakuwaga wagumu kwetu hivyo tumejiandaa kwa ajili ya hilo mimi pamoja na uongozi na wachezaji kwa ujumla,” alisema.

Mechi ya mwisho Yanga dhidi ya Polisi katika Uwanja huo waliibuka na ushindi wa tabu wa goli 1-0 katika msimu uliopita.

SOMA NA HII  FT: YANGA 3-0 MTIBWA SUGAR ....AZIZ KI AFUFUKIA KWENYE 'JUA LA UTOSI'...MAMBO YA KICONGO YAFANYA KAZI KWA MKAPA...