Home Uncategorized NYOTA LYON AMTUMIA UJUMBE BEKI KISIKI WA LIVERPOOL

NYOTA LYON AMTUMIA UJUMBE BEKI KISIKI WA LIVERPOOL


NYOTA wa Klabu ya Lyon,  Memphis Depay amemtumia ujumbe beki kisiki wa Liverpool ambaye kwa sasa anatibu majeraha yake aliyoyapata kwenye mchezo  wa Ligi Kuu England dhidi  Everton wakati wakilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2.

Beki huyo anatarajiwa kuwa nje kwa muda wa msimu mzima akitibu jeraha lake la goti huku Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wakiwa na hesabu za kumpata mbadala wake kwenye usajili wa Januari. Depay alituma ujumbe huo wakati timu yake ya Lyon ikishinda mabao 4-1 dhidi ya Monaco mchezo wa Ligue 1.

Baada ya kufunga bao lake la kwanza dakika ya 12, Depay alionyesha maneno yaliyoandikwa kwenye tisheti yake ambayo yaliandikwa kwamba nakuombea urejee kwenye ubora wako kaka Dijk. 


Mabao mengine ya Lyon yalifungwa na Kari Ekambi aliyefunga mabao mawili dakika ya 34 na 44 na lingine lilifungwa na Houssein Aouar dakika ya 41 kwa penalti na lile la Monaco lilifungwa na Wissam Yedder dakika ya 48 kwa penalti


Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Parc Olympique Lynnais nyota wa Klabu ya Lyon Melvin Bard alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 89.

SOMA NA HII  AMRI SAID WA MBEYA CITY AFUTWA KAZI