Home Uncategorized WACHEZAJI SIMBA MTEGONI, ATAKAYEKIUKA ADHABU JUU YAKE INAMUHUSU

WACHEZAJI SIMBA MTEGONI, ATAKAYEKIUKA ADHABU JUU YAKE INAMUHUSU

SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wachezaji wa Simba kabla ya kuvunja kambi walifanyiwa vipimo vya uzito hivyo atakayeongezeka kilo ghafla hatua itachukuliwa.

Hatua hiyo imefikiwa kutokana na kambi za timu kuvunjwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Serikali ilizuia mikusanyiko isiyo ya lazima.

Matola amesema:”Tunatambua kwamba kwa mazingira ambayo tupo itakuwa ngumu kuwadhibiti wachezaji kwa upande wa vyakula ila tuliwapima uzito hilo lipo kwenye rekodi.

“Mchezaji ambaye ataonekana ameongezeka kilo ghafla itakuwa ni rahisi kutambua kwamba hakufuata program aliyopewa hivyo hatua juu yake itachukuliwa,” .

SOMA NA HII  AMUNIKE: TUTAFANYA MAAJABU MISRI