Home Uncategorized AMUNIKE: TUTAFANYA MAAJABU MISRI

AMUNIKE: TUTAFANYA MAAJABU MISRI

KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Emmanuel Ammunike amesema kuwa kwa sasa kikosi kipo sawa kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Zimbabwe utakaopingwa nchini Misri.

Kwa sasa kikosi cha Stars kipo nchini Misri ambapo kimeweka kambi maalumu ikiwa ni maandalizi kuelekea michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza Juni 21 na wameanza kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri.

Amunike amesema kuwa mchezo wa kirafiki waliocheza dhidi ya Misri licha ya kufungwa bao 1-0 umewafumbua macho na kuona mapungufu yao hivyo kuelekea mchezo wa kesho watafanya maajabu.

“Mchezo wetu dhidi ya Misri umetufumbua macho na tumejua mapungufu yetu hivyo tutayafanyia kazi kwenye mchezo wetu wa kesho dhidi ya Zimbabwe, hii itatufanya tuwe bora zaidi,” amesema Amunike.

SOMA NA HII  MALENGO YA BIASHARA UNITED NI TANO BORA, YAWAOMBA WADAU KUIPA SAPOTI