LEO Jumamosi, Juni 15, Kubwa Kuliko itazinduliwa rasmi ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga jijini Dar es Salaam na wanachama pamoja na viongozi wa Yanga lengo likiwa moja kuichangia timu.
Ikumbwe kwamba mchakato huu kwa mara ya kwanza ulizinduliwa na Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera makao makuu ya nchi, Dodoma.
Katibu wa Kamati ya Hamasa ya Yanga, Deo Muta amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika litaanza saa nne asubuhi hadi saa kumi kamili jioni.
Muta amesema kuwa, tamasha hilo linakwenda kuibadilisha Yanga na kutengeneza historia ndani ya timu hiyo katika kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kujiendesha.
“Wadau mbalimbali tumewaarika katika tamasha hili kubwa la kihistoria la Kubwa Kuliko ambalo litafanyika kwa siku nzima ya Jumamosi hii wakiwemo wasanii wa Bongo Muvi na Bongo Fleva, wachezaji wa zamani, wanachama na mashabiki.
“Tamasha litakuwa ‘live’ likirushwa na kituo cha Televisheni cha Azam TV, pia kwa wale watakaokuwa mbali na TV, tumewarahishia kwa kuweza kuangalia kwa njia ya simu au ‘laptop’ kwa kutumia mfumo wa online wa ‘Pay Per View,”amesema Muta.