Home Uncategorized JIPYA LAIBUKA JUU YA USAJILI WA BWALA SIMBA

JIPYA LAIBUKA JUU YA USAJILI WA BWALA SIMBA


Imeripotiwa kuwa klabu ya Simba imegoma kutoka kiasi cha fedha ambacho Nkana Red Devils wanakitaka ili kumuachia mchezaji wao Walter Bwalya.

Taarifa za ndani zinasema Nkana wanahitaji kiasi cha shilingi milioni 800 za kitanzania jambo ambalo limekuwa ni gumu kuzitoa.

Uongozi wa juu wa Simba kupitia kwa Ofisa Mtendaji wake, Crescentius Magori, umesema kwa fedha hiyo hawataweza kumsajili Bwalya na badala yake watamsaka mchezaji mwingine.

Imeelezwa kuwa Magori amefunguka kwa kusema Nkana wanadai fedha kubwa tofauti na uwezo wa mchezaji mwenyewe ulivyo kitu ambacho kinaleta ugumu kumnunua.

Tetesi za Bwalya kutua Simbazimeanza muda mrefu lakini mpaka sasa pande zote mbili hazijaelewana juu ya usajili wake.

SOMA NA HII  NYOTA HAWA WALIZIPA TABU SIMBA NA YANGA, SASA WANAPETA KWENYE TIMU MPYA