Home Uncategorized HIKI NDICHO KILICHOMPONZA CHIRWA, SINGANO, LYANGA KUPIGWA CHINI AZAM FC

HIKI NDICHO KILICHOMPONZA CHIRWA, SINGANO, LYANGA KUPIGWA CHINI AZAM FC


IMEELEZWA kuwa sababu kubwa ya kocha Ettiene Ndayiragije kuwatema wachezaji nane wa kikosi hicho ni pamoja na kutoridhishwa na uwezo wa wachezaji hao pamoja na nidhamu.

Azam FC leo wanaingia kambini rasmi kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kagame inayotarajiwa kuanza mwezi Julai nchini Kagame wakiwa ni mabigwa watetezi.

Wachezaji hao ni pamoja na Obrey Chirwa ambaye tangu mwanzo aligoma kuongeza mkataba hali iliyofanya aachwe kwa kigezo cha nidhamu moja kwa moja huku Tafadzwa Kutinyu yeye akiwa amepata mkataba wa kukipiga Horoya FC.

 Ramadhan Singano, Steven Kigue, Hassan Mwasapili,  Daniel Lyanga, Joseph Kimwaga, Enock Atta hawa wote mikataba yao imemalizika na kocha hakukubali kuwaongezea mkataba.

SOMA NA HII  KOCHA MRUNDI AKUBALI MUZIKI WA KISINDA,AMTABIRIA MAKUBWA