Home Habari za michezo GAMONDI AWAPA MSTAA YANGA KIBARUA KINGINE

GAMONDI AWAPA MSTAA YANGA KIBARUA KINGINE

Habari za Yanga SC

Mchora ramani za ushindi ndani ya kikosi cha Yanga, Miguel Gamondi amewapa majukumu mengine mastaa wake wakiongozwa na muunganiko wake matata wa PAM unaowajumuisha Pacome Zouzoah, Aziz KI na Maxi Nzengeli kuendeleza kasi yao.

Ikumbukwe kwamba PAM imehusika kwenye mabao ya kufunga 18 ambapo Pacome ana mabao manne huku Aziz KI na Maxi hawa wakiwa wametupia mabao sabasaba kila mmoja.

Gamondi alisema kuwa jukumu la wachezaji wote ni kufanya kazi kwa ushirikiano na kuwa na kiu ya kupata ushindi kwenye kila mchezo ambao wanacheza.

“Ukianza na viungo waliopo ndani ya timu kuanzia Maxi, Aziz hawa wote ni muhimu kushirikiana kupata matokeo kwenye mechi ambazo tunacheza na hilo linawezekana kwa kuwa kila mmoja anafurahia anachokifanya.

“Tunapenda kuona namna ambavyo Pacome anafanya kazi kwa ushirikiano na wachezaji wengine kwani hili ni jukuumu la kila mchezaji. Tunacheza kupata matokeo na hilo linaonekana hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Gamondi.

SOMA NA HII  MO DEWJI: UNAMTAKA MIQUISSONE, SUBIRI MIAKA MITATU NA NUSU...