Home Habari za michezo METACHA NDIO BASI TENA YANGA….GAMONDI ‘ASIMAMIA UKUCHA’ JAMBO LAKE…

METACHA NDIO BASI TENA YANGA….GAMONDI ‘ASIMAMIA UKUCHA’ JAMBO LAKE…

Habari za Yanga SC

Imeelezwa kuwa mlinda lango Metacha Mnata bado hajarejea kikosini baada ya kocha Miguel Gamondi ‘kumuwekea ngumu’ kurejea kikosini hapo kwa kile kilichoelezwa kuchelewa kurudi kutoka kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

Nidhamu ya wachezaji ni kipaumbele cha kwanza cha Gamondi na amekuwa mkali kwa wachezaji ambao hawafuati taratibu zilizowekwa.

Metacha alichelewa kujiunga na kikosi cha Yanga baada ya majukumu ya timu ya Taifa na alitakiwa kutoa maelezo kwani hakutoa sababu mapema kwa nini amechelewa.

Kwa sasa bado hayuko sehemu ya kikosi akikosa mechi tatu zilizopita kwenye ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc, Geita Gold na Azam Fc.

Djigui Diarra na Aboutwalib Mshery ndio walinda lango wanaoonekana kwenye mazoezi ya Yanga.

SOMA NA HII  KISA SARE TATU MFULULIZO...MANARA AFUNGUKA MAMBO YALIVYOKUWA 'MTIFUANO' YANGA...