Home Uncategorized ANTOINE GRIEZMANN AINGIA KWENYE REKODI YA WACHEZAJI GHALI

ANTOINE GRIEZMANN AINGIA KWENYE REKODI YA WACHEZAJI GHALI


ANTOINE Griezmann amejiunga na Barcelona kwa kusaini kandarasi ya miaka mitano akitokea kikosi cha Atletico Madrid.
Nyota huyo mwenye miaka 28 anayekipiga timu ya Taifa ya Ufaransa ambao ni mabingwa wa kombe la Dunia amesaini dili hilo ambalo limefikisha gharama ya milioni 800 Euro ikiwa ni gharama ya ada ya usajili wake.
Atletico Madrid bado hawana furaha kumuacha mchezaji wao kujiunga na klabu ya Barcelona kutokana na umuhimu wake ndani ya kikosi chao.
Griezmann anaingia kwenye rekodi ya wachezaji sita wa gharama kumwaga wino ikiwa ni pamoja na  Neymar, Kylian Mbappe, Philippe Coutinho, Joao Felix na Ousmane Dembele.
SOMA NA HII  SIMBA NA YANGA ZACHONGANISHWA NA MTUPIAJI HUYU