Home Uncategorized MARIO BALOTELLI APATA DILI LA MAANA PARMA FC

MARIO BALOTELLI APATA DILI LA MAANA PARMA FC


MARIO Balotelli ambaye ni straika huenda akatua kwenye kikosi cha Parma baada ya kumalizana na kikosi cha Marseille.

Mkurugenzi wa klabu hiyo, Daniele Faggiano ameweka wazi kwamba wanahitaji saini ya nyota huyo baada ya kukosa saini ya nyota wa Roma, Daniele De Rossi kutokana na kutaka mshahara mkubwa.

Balotelli nyota wa zamani wa Manchester City na AC Milan mkataba wake umemalizika ndani ya klabu yake ya Marseille na sasa ni mchezaji huru.

Balotelli alifunga mabao nane baada ya kutua kikosini hapo kwenye mechi 12 alizocheza akitokea klabu ya Nice.

SOMA NA HII  SIMBA WAJANJA KWELI WAMUWAHI YULE MTUPIAJI ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA