Home Uncategorized KIUNGO POLISI TANZANIA ATUMA UJUMBE KWA WATANZANIA WOTE KUOMBEANA DUA

KIUNGO POLISI TANZANIA ATUMA UJUMBE KWA WATANZANIA WOTE KUOMBEANA DUA


BARAKA Majogoro, kiungo wa Polisi Tanzania amesema kuwa ni muhimu kwa kila mmoja kwa sasa kuomba dua wakati huu wa kipindi cha maambukizi ya Virusi vya Corona.


Majogoro amesema kuwa kwa sasa ni wakati wa kuungana katika kupambana na Virusi vya Corona ili hali irejee kama ilivyokuwa zamani.

“Muhimu kukumbuka kuombeana kila mmoja kwa wakati wake na kuchukua tahadhari ili kuwa salama kwani hali sio shwari kwa sasa, imani yangu tukifuata taratibu tutakuwa kwenye wakati mzuri wa kuishinda hii vita,” amesema.

Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa na Serikali ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia kwa sasa.
SOMA NA HII  HESABU ZA FOUNTAIN GATE NI NDEFU KWELI