Home Simba SC AJIBU ATAJWA KUSEPA SIMBA MSIMU UTAKAPOISHA

AJIBU ATAJWA KUSEPA SIMBA MSIMU UTAKAPOISHA


 IMEELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Simba, Ibrahim Ajibu msimu utakapomeguka atasepa ndani ya kikosi hicho ili akapate changamoto mpya.

Ajibu alijiunga na Simba akitokea Yanga kwa dau lililotajwa kuwa milioni 70 ambapo amekuwa hana nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza.

Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuhitaji saini yake ni timu yake ya zamani Yanga huku Azam FC wao wakigomea kuhitaji saini yake kwa kile kilichoelezwa kuwa hana sifa ya kucheza katika kikosi hicho kwa kuwa hana namba kikosi cha kwanza cha Simba.

Hivi karibuni ilielezwa kuwa nyota huyo amemalizana na mabosi wa Yanga hivyo ni suala la muda kurudi ndani ya kikosi hicho ambacho alikuwa nahodha zama za Mwinyi Zahera.

Pia aligoma kutolewa kwa mkopo kama ilivyokuwa kwa mshikaji wake Charlse Ilanfya ambaye yupo zake akipambana ndani ya KMC wana Kino Boys.

Ofisa Habari wa Yanga kupitia Spoti Xtra alieleza kuwa hawana mpango wa kufanya jambo hilo kwa sasa.

SOMA NA HII  VIATU VYA ONYANGO TARATIBU MIKONONI MWA MZAWA JUMA