Home news VIATU VYA ONYANGO TARATIBU MIKONONI MWA MZAWA JUMA

VIATU VYA ONYANGO TARATIBU MIKONONI MWA MZAWA JUMA


 MZAWA, Keneddy Juma, mwili jumba beki wa mpira taratibu anaanza kuwa fiti kila anapotokea benchi kwenye mechi za ushindani ndani ya Simba licha ya kutoaminika mara kwa mara mbele ya Didier Gomes ambaye ni Kocha Mkuu.

Ikumbukwe kwamba Keneddy ni mshikaji asiyependa kuzungumza kwa maneno ila matendo na kila anapopata mpira rekodi zinaonyesha sio mtu wa mambo mengi na pasi anazopenda kuzitoa ni zile pasi fupifupi na ndefu huwa anamuachia Pascal Wawa.

Kwenye mechi mbili za Gomes, Keneddy akitokea benchi aliweza kuonyesha kile alichonacho kwa kutimiza majukumu yake vizuri ilikuwa ni ile ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs Mei 22, wakati Simba ikishinda mabao 3-0.

Beki huyo alitokea benchi na aliyeyusha dakika 56 baada ya Onyango kuumia na aliweza kufanya hivyo kwa kuzuia mashambulizi ya mshambuliaji msumbufu na wa bei ghali Samir Nurkovic. Aliweza kufanya hivyo juzi Septemba 25 alipoingia kuchukua nafasi ya Onyango.

Aliweza kuvaa viatu vizuri vya Onyango kwa kuwa aliweza kutuliza mashambulizi na kutibua mipango ya Fiston Mayele, Heritier Makambo waliokuwa kwenye kasi yao wakati Simba ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kupoteza taji la Ngao ya Jamii.

Kwenye ligi msimu wa 2020/21 kwenye mechi 34 ni mechi 16 aliweza kucheza na alikosekana katika jumla ya mechi 18.

Ni miongoni mwa wachezaji ambao leo Septemba 27 wametajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen.


SOMA NA HII  KUHUSU KIMATAIFA SIMBA ,YANGA NJIA HII HAPA