Home Habari za michezo KUHUSU KIMATAIFA SIMBA ,YANGA NJIA HII HAPA

KUHUSU KIMATAIFA SIMBA ,YANGA NJIA HII HAPA

Habari za michezo

Simba SC na Young Africans siyo ishu tena kushinda ugenini katika michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’, isipokuwa zimeshauriwa kuweka nguvu katika mataji, ili kuandika historia.

Wachezaji wa zamani wa timu hizo wanaona ni wakati wa kuchukua mataji ya CAF wakitolea mfano wa Young Africans ilivyotinga fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger msimu uliopita.

Kocha wa zamani wa Simba SC, Abdallah Kibadeni amesema kuweza kupata matokeo ugenini kwa kujiamini kunatafsiri kuwa hakuna linaloshindikana.

“Mfano Young Africans haikuwa bahati yao michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu uliopita, ilifanya vizuri hadi kucheza fainali, hivyo klabu hizo kongwe inawezekana kabisa zikafanikisha taji hilo,” amesema.

Kipa wa zamani wa Young Africans, Benjamin Haule aamini kuna kila sababu wa klabu hizo kongwe kuandika rekodi akitoa sababu za usajili dhidi ya timu wanazoshindana nazo kwenye michuano hiyo.

“Simba SC na Young Africans zinasajili mastaa dhidi ya timu wanazoshindana nazo CAF, mfano Stephen Aziz Ki wa Young Africans, kwa Simba SC Moses Phiri.

Hao ni baadhi tu, ubora wa mastaa unaweza kuziwezesha kutwaa ubingwa siku za usoni,” amesema.

SOMA NA HII  FEISAL SALUM LEO MKWAWANI KUNACHIMBIKA , YANGA WAJIPANGE