Home Habari za michezo YANGA JANJA NYINGI SANA WATUMIA MBINU HII

YANGA JANJA NYINGI SANA WATUMIA MBINU HII

Habari za Yanga leo

Wakati baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao hawajaitwa timu zao za taifa wakitarajia kuondoka kesho Jumanne kwenda Algeria mabosi wa timu hiyo tayari umemtanguliza mmoja wa viongozi kwenda kuweka sawa mambo.

Yanga inatarajia kuondoka mafungu mawili, huku wale waliopo timu za taifa wakiungana na wenzao juu kwa juu baada ya kumaliza majukumu yao ya taifa. Arena express limepenyezewa taarifa, mmoja wa kiongozi (jina tunalo) ameondoka alfajiri ya kuamkia jana kwa lengo la kwenda kuweka mazingira sawa kwa kuhakikisha anaandaa sehemu ya timu kufikia huku akiweka mazingira mazuri ya usafiri wa kuwapokea wachezaji.

Nyota wa kigeni ambao wapo nje ya timu na wataungana na wenzao juu kwa juu ni Dijgui Diarra, Khalid Aucho na Stephane Aziz Ki, huku wale wazawa waliopo Stars ni Abutwarib Mshery, Job, Mudathir, Bacca, Mwamnyeto na Nickson Kibabage.

SOMA NA HII  MANARA AWATOLEA UVIVU TFF KISA CHAMA, AZIZ KI.... ISHU IKO HIVI