Home Habari za michezo KIPA ORLANDO AIGOPA SIMBA…AWATONYA HAYA WYDAD CASABLANCA

KIPA ORLANDO AIGOPA SIMBA…AWATONYA HAYA WYDAD CASABLANCA

KIPA ORLANDO AIGOPA SIMBA...AWATONYA HAYA WYDAD CASABLANCA

Kipa wa Orlando Pirates Richard Ofori amewapa tahadhari Wydad Casablanca na kuwaambia wawe makini wanapotua kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Wydad ambao ni mabingwa watetezi wanatarajia kucheza na Simba kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Aprili 22,
kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam baada ya droo kuchezeshwa nchini Misri wiki iliyopita.

Ofori ambaye alikuwa langoni wakati Orlando ilipoitoa Simba kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mkapa na kwenda Afrika Kusini kulala kwa 1-0 na hivyo Wekundu wa Msimbazi
kutupwa nje kwa penalti 4-3.

Katika mchezo wa pili nchini Afrika Kusini, Simba ililazimika kumaliza pungufu baada ya mshambuliaji wao Chris Mugalu kupewa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi beki wa Pirates Olisa Ndah.

Ofori ambaye alifanikiwa kufunga penalti moja kwenye ushindi huo, akizungumza kwenye kipindi maarufu cha Soccer Afrika juzi, alisema Wydad wanatakiwa kuwa makini wanapokwenda Dar es Salaam na wasiamini kuwa utakuwa mchezo rahisi kwao.

“Nilikwenda pale mwanzo hakuna aliyekuwa anafahamu ni sehemu ya namna gani, lakini nataka niseme kucheza pale na kupata ushindi siyo jambo rahisi.

“Wydad wanatakiwa kufahamu kuwa Simba ina uwanja mzuri, lakini pia ina mashabiki wengi wenye nguvu wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, hili ni jambo ambalo wanatakiwa kulichukulia kwa umakini sana, sidhani kama watakutana na mchezo rahisi pale,” alisema kipa huyo raia wa Ghana.

Katika mchezo wa Afrika Kusini, Ofori alifanikiwa kuokoa penalti iliyopigwa na Jonas Mkude huku ile ya Henock Inonga ikigoga mwamba na kuwafanya Simba watupwe nje.

Hii ilikuwa mara ya pili mfululizo Simba wanatupwa nje na timu ya Afrika Kusini baada ya mwaka mmoja nyuma kufungwa jumla ya mabao 4-3 na Kaizer Chiefs kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuchapwa 4-0 Afrika Kusini na kushinda 3-0 kwenye Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  KILA MMOJA ASHINDE YAKE..... KIGALI NZIMA YARINDIMA MAXI AAHIDI SHANGWE...... SIMBA YAAHIDI KUISHANGAZA DYNAMO KWAO