Home Habari za michezo YANGA WAKOMAA NA PACHA WA NZEGELI…. ISHU IKO HIVI

YANGA WAKOMAA NA PACHA WA NZEGELI…. ISHU IKO HIVI

Klabu ya Union Maniema imenogewa na biashara na Yanga na sasa iko kwenye hatua za mwisho kumwachia winga fundi ambaye alikuwa pacha wa Maxi Nzengeli.

Kocha wa Union Maniema ya DR Congo, Papy Kimoto ambayo ametoka Maxi ambayo Yanga imeshachukua wachezaji wanne amefichua kwa sasa ameacha kumtumia kwa muda winga wake Basiala Agee akijua kwamba wakati wowote anatimkia kwa mabingwa hao wa Tanzania.

Kocha Kimoto akizungumza na simu na Mwanaspoti amefichua tayari uongozi wa Maniema umeshamjulisha kwamba biashara hiyo iko kwenye hatua za mwisho kumalizika sababu iliyomfanya kumuondoa kwenye mipango yake.

Kwenye Ligi ya Kongo sasa Basiala amefanikiwa kufunga mabao matano na kutoa asisti tano huku akiwa amekosa mechi mbili za mwisho kutokana na maaamuzi ya kocha wake huyo.

“Uongozi ulishaniambia unamuuza Yanga (Basiala), kwa hiyo sioni sababu ya kuendelea kumtumia sasa tutamchanganya tu naona hata yeye ameshajiandaa kuondoka hapa na sisi tunajiandaa na maisha mapya,”alisema Komoto.

“Kwa sasa namtumia mtu wa pili nyuma yake, tunapoteza mchezaji bora lakini kwa kuwa tunaingiza fedha hakuna shida tutatengeneza wengine taratibu.”

Akizungumzia ubora wake Kimoto alisema, Basiala ni winga anayejua kuwapangua mabeki lakini hatua mbaya ni kwamba anajua kufunga kwa mashuti makali na kupiga mipira ya adhabu.

Kocha huyo kipenzi cha mmiliki wa timu hiyo Jenerali Amissi Kumba alisema kabla ya Maxi kuuzwa Maniema ilisitisha muunganiko wa wawili hao ambao sasa wanaweza kukutana Yanga.

“Atakuja huko mtasikia vile mabeki watalia ni kijana mdogo bado ana nguvu ana mbio na kujua kupenya kwa mabeki ni mzuri sana waambie Yanga imepata mchezaji mwingine bora.

“Yule rais wao (Hersi Said) anaongea vizuri sana na Jenerali ndio maana unaona biashara na Yanga imekuwa rahisi sana, hapa kabla ya Maxi kwenda huko walikuwa pamoja kama mapacha tulikuwa na nguvu kubwa sana, watakwenda kushirikiana huko Yanga tena.”

Mwanaspoti lilimtafuta Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, lakini simu zake hazikupokewa.

SOMA NA HII  GAMONDI AWAANDAA MASTAA HAWA KUELEKEA MCHEZO WA CAF