Home Habari za michezo WAKATI YANGA WAKIFUNGA GOLI TANO TANO….MBRAZILI SIMBA ATAKA MAGOLI YA KROSI…

WAKATI YANGA WAKIFUNGA GOLI TANO TANO….MBRAZILI SIMBA ATAKA MAGOLI YA KROSI…

Habari za Simba SC

KOCHA mkuu wa Simba, Mbrazil Robert Oliveira ‘Robertinho’ amewaambia wachezaji wake kuhukikisha wanaweza kutumia vyema mpira ya krosi kuweza kufunga mabao katika kila mchezo ili kuweza kufikia malengo yao msimu huu.

Robertinho ametoa kauli hiyo, Simba ikiwa inakabiliwa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wanatarajia kuanzia hatua ya pili dhidi ya Power Dynamo ya Zambia huku wakiwa na michuano ya Supa ligi pamoja na michuano ya ndani ikiwemo Ligi Kuu Bara na kombe la FA.

Kocha huyo akiwa makini alitumia saa mbili kwa ajili ya kukiona kikosi cha timu hiyo kwa kufanyia kazi mazoezi ya mipira ya faulo lakini huku makipa wa timu hiyo akiwemo Ally Salim na Hussein Abel walionekana kuwa makini na mipira hiyo kwenye mazoezi ya juzi, Mo Simba Arena.

Wakati viungo na washambuliaji kufanyia kazi kile anachopewa katika mazoezi hayo naye kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula ameanza proglamu maalum ya mazoezi binafsi chini ya uangalizi wa daktari Edwin Kagabo.

Robertinho alisema kuwa licha ya safu yake ya ushambuliaji kuendelea kufunga katika kila mchezo lakini amewataka wachezaji wa timu hiyo kuweka nguvu ya kuweza kutumia vizuri nafasi za mipira ya krosi kuweza kufunga mabao.

Alisema timu yake inaendelea kuimarika zaidi licha ya kuwa na wachezaji wachache lakini anaamini kabla ya kukutana na Power Dynamos watakuwa vizuri zaidi, huku akisisitiza anahitaji kuona mipira ya kutenga.

“Mipango yetu ipo katika michuano iliyopo mbele yetu, tunaendelea na maandalizi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu licha ya kukosa baadhi ya wachezaji ambao wamekwenda katika timu zao za taifa lakini hatuwezi kukaa bila ya kuendelea na mikakati yetu.

Kikubwa ni kwamba tupo kwenye wakati mzuri kwa sababu timu inaweza kupata matokeo ya ushindi wakati wote na kutengeneza nafasi ingawa nataka kuona wakutumia vyema mipira ya krosi kuweza kufunga mabao ambayo itatusaidia kupiga hatua kubwa ya kupunguza presha ambayo itakuwa upande wetu, ” alisema Robertinho.

SOMA NA HII  AS ROMA NA MOURINHO WAWEKA HISTORIA HII MPYA ULAYA...KILA MMOJA KAMNUFAIKA MWENZAKE..YANI NIPE NIKUPE....