Home Habari za michezo BAADA YA KUUONA MZIKI WA EL-MERREKH….GAMOND AWASHTUA JAMBO YANGA…

BAADA YA KUUONA MZIKI WA EL-MERREKH….GAMOND AWASHTUA JAMBO YANGA…

Habari za Yanga SC

KOCHA mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi raia ni kama amewashtukia wapinzani wao katika Ligi ya Mabingwa Afrika, El- Emerreikh ya Sudan kwa kuamua kufuta mapumziko kwa wachezaji wa timu hiyo na kuingia kambini na kuanza maandalizi kuelekea katika mchezo huo.

Yanga imeanza msimu huu kwa mafanikio kutokana na kutoa vipigo vizito katika Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwa sasa wapo kwenye mapumziko ya wiki mbili kwa ajili ya kupisha michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa Afrika Afcon zinazotarajia kufanyika nchini Ivory Coast.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga inatarajia kucheza mchezo wa kwanza wa hatua ya pili ya kuwania kufuzu katika makundi ya michuano hiyo, Septemba 16, mwaka huu kabla ya mchezo wa marudiano unaotarajia kupigwa Septemba 30, mwaka huu jijini Dar.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya timu hiyo, zinaeleza kuwa Gamondi amegomea wachezaji kwenda kukaa mapumziko katika kipindi hiki cha kupisha michezo ya timu za taifa kutokana na ratiba ngumu iliokuwepo mbele yao.

Kocha huyo ambaye anatajwa aliwapa siku moja pekee kwa ajili ya mapimziko kabla ya juzi kwa wachezaji kurejea kambini na kuendelea na program zake kwa wachezaji ambao hawajaitwa kwenye timu zao za taifa ikiwa ni lengo la kujiandaa na mchezo wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El-Merreikh.

Kwa upande wa Gamondi alisema kuwa anaamini ana kikosi bora kina uwezo wa kupata matokeo katika mchezo wowote lakini hataki kuona wachezaji waende mapumziko yoyote kutokana na mashindano yaliokuwa mbele yao.

“Hakuna sababu ya kupumzika, tayari tulipumzika siku moja na tayari turejea uwanjani, tunatakiwa kufikia malengo yetu hivyo ni vyema tukaongeza nguvu katika kipindi hiki kuhakikisha tunafikia malengo yetu,” alisema Gamondi.

Aliongeza kuwa El-Merreikh ni timu nzuri ina wachezaji ambao wanaweza kuleta matokeo na hakuna umuhimu wachezaji kupumzika kwa sasa wanahitaji kufuzu na kucheza hatua ya makundi.

“Yanga haijawahi kufika makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, tunahitaji mapumziko ya ligi kuu kwa ajili ya kuendelea kutengeneza timu na kufanyia makosa yaliyojitokeza kwenye mechi zilizopita, ikiwemo kuruhusu bao au kusababisha penalti,” alisema Kocha huyo.

Yanga itacheza na El Mareikh baada ya kuitoa timu ya Asas FC ya Djibouti kwa jumla ya mabao 7-1 katika mchezo wa hatua ya awali, michezo yote ilichezwa katika Uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Msimu uliopita Yanga ilikuwa mshindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC), nyuma ya mabingwa USM Alger ya Algeria na kukosa taji hilo kwa kanuni ya bao la ugenini, ambapo walifungwa mabao 2-1 hapa nyumbani na wakashinda 1-0 ugenini.

Yanga iliangukia katika Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kipigo cha jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

SOMA NA HII  HUZUNI KUTANDA CHAMAZI...GAMONDI AKIRI KUPAMBANA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU...AMEFUNGUKA HAYA