Home Habari za michezo WAKATI PACOME AKIANZA ‘KUCHANGAYA’ YANGA….KOCHA WAKE WA ASEC MOMOSAS KAIBUKA NA HILI…

WAKATI PACOME AKIANZA ‘KUCHANGAYA’ YANGA….KOCHA WAKE WA ASEC MOMOSAS KAIBUKA NA HILI…

Habari za Yanga

Wakati Yanga ikitakata kwa furaha ya kiwango anachokionesha Kiungo wao mpya Pacome Zouzoua aliesajiliwa kutokea Asec Mimosas.

Kocha wa ASEC Mimosas Julien Chevalier ametoa kauli ya kushangaza akieleza kuwa uwezo ambao Mashabiki wa Yanga wameuona kwa Pacome na kuushangilia ni asilimia 40 tu ya Uwezo wake.

Akizungumza Julien Chevalier anasema;

“Kwa Usajili wa Pacome Zouzoua Yanga imepata fundi anayejua kufunga na kutengeneza nafasi za mabao, Huwa nalazimika kuangalia marudio ya mechi kadhaa za Yanga nikitaka kujua maendeleo ya Zouzoua, hapo Yanga wajue amecheza kwa asilimia 40 tu ya kiwango chake halisi”

“Namkumbuka sana Zouzoua, ni kijana wangu, watu hawajui hiyo timu iliyomsajili ilipomchukua wakati ule Aziz KI (Stephanie), tulimchukua Zouzoua kuziba nafasi yake na msimu wa kwanza alituonyesha kwanini tulimuamini, niliumia sana alipokuja kuniaga kwamba anaondoka kuja huko,”

“Akiwa sawasawa timu yake itakuwa na makali kwenye kiungo, ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa anaweza kufanya vitu ambavyo hata kocha ukashangaa ana ufundi sana akiwa na mpira nadhani klabu yake itafurahia sana. Kocha huyo alifurahishwa pia kuanza kwa kasi kwa beki wake Kouassi Yao akisema beki huyo ni kijana mdogo mwenye moyo wa mnyama mkali uwanjani.”

SOMA NA HII  AL MAREIKH HAWA HAPA NCHINI KWAAJILI YA YANGA