Home Habari za michezo YANGA WATAJA WATAKAO PATA TIKETI ZA BURE MECHI YA FAINAL KESHO…UTARATIBU NI...

YANGA WATAJA WATAKAO PATA TIKETI ZA BURE MECHI YA FAINAL KESHO…UTARATIBU NI HUU…

Habari za Yanga SC

UONGOZI wa Yanga umesema baada ya kufanya maandalizi mazuri pande zote mbili benchi la ufundi na viongozi wako tayari kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa fainali ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF) dhidi ya USM Alger ya Algeria.

Yanga jumapili ya wiki hii wanatarajia kucheza mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger ya Algeria katika mchezo unaotarajia kupigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, saa 10:00 alasiri.

Akizungumza na makao makuu ya Yanga jana, Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe alisema kikosi kinaendelea vizuri na maandalizi ya mchezo wao huo wa fainali kwa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri nyumbani kwa kumaliza mechi hiyo katika dimba la Benjamin Mkapa.

“Wiki hii ya fainali ya CAF, sio ya mihemuko na viongozi wote wako makini na maandalizi ya mchezo huo kujiandaa jinsi ya kushinda hiyo mechi nyumbani kabla ya kwenda kumalizia ugenini.

Hii ni mara ya kwanza kucheza fainali, viongozi wako makini sana na kutuliza akili ili kufanikisha malengo yetu ya kushinda nyumbani na kupata matokeo ugenini ili Juni 4, mwaka huu tukirudia na kombe la Afrika,” alisema Kamwe.

Aliongeza kuwa kwa sasa wanatarajia kupata wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali huku makadirio ya wageni kutoka CAF wanatarajia kupata watu zaidi ya watu 200.

Kamwe alisema mchezo wa marudiano ambao wanaenda kucheza Algeria, wanatarajia kutumia ndege waliopewa na Mh. Rais Samia ambayo inawapeleka na kuwasubiri kwa siku zote na kurejea na kombe la Afrika.

“Sasa twende zetu Algeria na lengo kubwa kutafuta mashabiki kwenda nao nchini humo na utaratibu ni ule ule wa awali wa kucheza bahati nasibu ili kupata nafasi ya kwenda nchini humo,” alisema msemaji huyo.

Naye Mkurugenzi wa wanachama na mashabiki wa Yanga, Haji Mfikirwa alisema kwa sasa ni wakati mahususi kwa mashabiki na wanachama wa Yanga kujitikezea kwa wingi uwanjani katika mchezo huo wa fainali.

Alisema kuhusu tiketi wamepokea nyingi tofauti na awali ambazo walikuwa wamepokea katika muchezo ya nyuma ambapo walipokuwa wakifanya harambee katika mashindano hayo.

“Hadi sasa tumepokea jumla ya tiketi elfu 18,213 kutoka kwa wadau mbalimbali akiwemo Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu na tumeanza mchakato wa kuzigawa kwa wanafunzi wa vyuo na vingine tunasubiri utaratibu mwingine wa kufikia wanachama wetu na mashabiki,” alisema Mfikirwa.

Aliongeza kuwa uongozi juu wa Yanga umetafakari na kuona namna gani ya kuona kina nani hizo tiketi zitawafikia ili watanzania kujitokeza uwanjani, kwa wale wa mikoani ambao wanasafiri masafa kuja kuangalia timu yao hao nao wamefikiriwa kwa kuleta usawa kwa wanayanga wote kupata haki sawa kuja kushuhudia timu yao.

“Kupitia matawi ya Yanga wote kutoka mikoa mbalimbali wanakuja katika hii mechi, hivyo tumefanya utaratibu wa kutoa tiketi ambazo tumezipokea, ndani ya siku hizi mbili tutajua utaratibu wa kugawa vipi hizo tiketi kwa wanachama na mashabiki wetu,” alisema Mkurugenzi huyo wa wanachama na mashabiki wa Yanga.

SOMA NA HII  HERSI ATOBOA SIRI YAYANGA NA MAKAMPUNI HAYA