Home Habari za Yanga Leo YANGA YAJIPANGA KUIPASUA KAIZER CHIEF…GAMONDI ATOA NENO

YANGA YAJIPANGA KUIPASUA KAIZER CHIEF…GAMONDI ATOA NENO

HABARI ZA YANGA-NABI

MABINGWA Mara 30 wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2023/24 Yanga wapo tayari kuwakabili Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa Toyota Cup.

Klabu ya Yanga ipo katika viwanja vya St Stithians, Johannesburg, Afrika Kusini chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuinoa timu hiyo kwenye mechi za ushidani.

Julai 28 2024 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2024/25 ambao unatarajiwa kuanza Agosti 16.

Miongoni mwa wachezaji waliopo katika kikosi ni Clatous Chama, Pacome, Aziz Ki, Prince Dube, Aboutwalib Mshery, Kibwana Shomari, Yao, Jean Baleke.

Kwenye mechi mbili zilizopita za kirafiki, Yanga ni nyota wawili walipata nafasi ya kufunga ambao ni Jean Baleke kwenye mchezo wa kwanza na mchezo wa pili ni Prince Dube alipata nafasi ya kufunga.

Kocha wa klabu hiyo Miguel Gamondi amebainisha kuwa mechi za kirafiki ambacho kinatazamwa kwa ukaribu ni namna wachezaji wanavyotumia maelekezo wanayopewa ili kuwa imara na kufanyia kazi makosa yao zaidi kuliko kufikiria ushindi.

“Kwenye mechi zetu za kirafiki kikubwa ambacho tunakitazama ni namna wachezaji wanavyocheza na kutumia maelekezo ambayo tunayafanya katika eneo la mazoezi hivyo kushinda kwetu sio kipaumbele kikubwa.’

Yanga itacheza mchezo huo wa kirafiki siku ya Jumapili na kuanza safari ya kurudi nchini,  ili kujiandaa na Kilele cha Wiki ya Wananchi Agosti 4.

SOMA NA HII  SPIDERMAN CAMARA AMTISHIA DIARRA...MWENYEWE AFUNGUKA