Home Habari za michezo AL MAREIKH HAWA HAPA NCHINI KWAAJILI YA YANGA

AL MAREIKH HAWA HAPA NCHINI KWAAJILI YA YANGA

Habari za Yanga

Wapinzani wa Yanga katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Merrikh ya Sudan, wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam, kesho Jumatano.

Msafara wa kikosi hicho unatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar majira ya 9:00 Alasiri, ukitokea Rwanda kwa Shirika la Ndege la RwandAir.

Ofisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe, amebainisha kwamba: “Wenzetu Al Merrikh wataingia kesho majira ya saa tisa kamili alasiri, kwa Shirika la Ndege ya Rwanda.

“Tumesikia kauli za Kocha wa Al Merrikh anasema kuwa Yanga SC inaogopeka Afrika. Sisi tumesoma Cuba, tunamwelewa, hawezi kutuchota, tutauchukulia mchezo kwa umakini mkubwa.

“Kocha wa Al Merrikh amesema pia anakuja kufunguka hapa, kwetu sisi ni taarifa njema kwa sababu mnara haukusoma Rwanda, hivyo tukipishana nao itakuwa fursa ya kusimamisha mnara.”

SOMA NA HII  BAADA YA UKIMYA MWINGI ONYANGO AFUNGUKA HAYA