Home Uncategorized SIMBA YAWAPIGA MKWARA MZITO WAZIMBABWE

SIMBA YAWAPIGA MKWARA MZITO WAZIMBABWE


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa wapinzani wao FC Platinum itakuwa ngumu kutoka kwenye mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Januari 6, Uwanja wa Mkapa.

Simba chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ina kibarua cha kupindua meza kwenye mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ili iweze kutinga hatua ya makundi.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila kwa namna yoyote ile itakuwa ngumu kwa wapinzani wao kutoka.

“Mashabiki wetu ambao ni mastaa namba moja ndani ya timu yetu tunawaomba wajitokeze kuipa sapoti timu yetu kwa kuwa hakuna namna mpinzani wetu hatoki pale kwa Mkapa.

“Maandalizi na mipango kuhusu mchezo wetu wa marudio yapo vizuri tunasubiri muda ufike ili tuweze kutoa burudani kwa mashabiki pamoja na kuliwakilisha taifa letu la Tanzania kimataifa,” amesema.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe, Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 inakibarua cha kusaka ushindi wa mabao zaidi ya mawili ili kusonga mbele.


Tayari wapinzani wa Simba, FC Platinum wametia timu ndani ya ardhi ya Dar, jana Desemba 2 ambapo wameweka wazi kwamba wamekuja kwa kazi moja ya kusaka ushindi.


SOMA NA HII  HAWA HAPA WANAOMBEBA FEI TOTO YANGA