Home Habari za michezo AZIZ KI AENDELEA KUMUONYESHA UBABE CHAMA…TFF WATHIBITISHA KWA TAARIFA HII

AZIZ KI AENDELEA KUMUONYESHA UBABE CHAMA…TFF WATHIBITISHA KWA TAARIFA HII

AZIZ KI AENDELEA KUMUONYESHA UBABE CHAMA...TFF WATHIBITISHA KWA TAARIFA HII

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Ki Aziz ameteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Aprili wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2023/2024, huku Miguel Gamondi wa Yanga akichaguliwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo.

Ki amewashinda Kipre Junior wa klabu ya Azam na Joseph Guede wa Yanga alioingia nao fainali kwenye mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).

Kwa mwezi Aprili, Ki alionesha kiwango kikubwa na kuwa msaada kwa timu yake katika ushindi wa michezo mitatu kati ya minne ambayo timu hiyo ilicheza, hivyo Yanga kukusanya alama 10 na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi.

Yanga iliifunga Singida FG mabao 3-0, ikaifunga Simba mabao 2-1, ikaifunga Coastal Union bao 1-0 kisha ikatoka 0-0 na JKT Tanzania. Ki alicheza jumla ya dakika 359 za michezo hiyo.

Kwa upande wa Gamondi aliiongoza Yanga kukusanya alama 10 katika michezo minne iliyocheza, ikishinda mitatu na sare moja, hivyo kuendelea kuongoza ligi hiyo yenye timu 16. Gamondi amewashinda Bruno Ferry wa Azam na Malale Hamsini wa JKT Tanzania alioingia nao fainali.

Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam, Amir Juma kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Aprili kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Imetolewa na;
Idara ya Habari na Mawasiliano
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Mei 5, 2024

Chairman: Steven J. Mnguto Email: s.mnguto@ligikuu.co.tz CEO: Almasi J. Kasongo Email: a.kasongo@ligikuu.co.tz

SOMA NA HII  KIBU AWAINGIZA VITANI SIMBA NA YANGA...MRITHI WA LOMALISA YUPO NJIA PANDA