Home Habari za michezo YANGA KUKIPIGA DODOMA DHIDI YA TABORA

YANGA KUKIPIGA DODOMA DHIDI YA TABORA

Tetesi za Usajili Bongo

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imefanya mabadiliko ya uwanja wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Tabora United dhidi ya Yanga SC

Mchezo huo namba 110, ambao timu Yanga SC itakuwa ugenini, sasa utachezwa Desemba 23, 2023, saa 1:00 Usiku kwenye Uwanja wa Jamhuri uliopo Dodoma.

Awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa Desemba 22, 2023, saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi uliopo mkoani Tabora.

Kwa mujibu wa TPLB, sababu za mabadilko hayo ni Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kufungiwa na Kamati ya Leseni za Klabu ya TFF.

SOMA NA HII  MZIKI HUU WA YANGA BADO HAMJASEMA...... AL MAREIKH HAWAAMINI MACHO YAO