Home kimataifa TUCHEL AITAKA SAINI YA ERIKSEN WA INTER MILAN

TUCHEL AITAKA SAINI YA ERIKSEN WA INTER MILAN

IMERIPOTIWA kuwa Chelsea ipo na uwezekanao mkubwa wa kumpata Christian Eriksen wa Inter Milan na kurejea ndani ya Ligi Kuu England kwa kubadilishana na Jorginho ili kuwa sehemu ya kukamilisha dili hilo.

Mtikisiko wa kuipata saini ya kiungo huyo umewakuta pia Tottenham ambao wanahitaji kuipata saini yake ili wamrejeshe kwenye timu yake ya zamani.

 Jorginho wa Chelsea amewekwa kwenye mpango wa kupelekwa ndani ya Inter Milan inayoshiriki Serie A ili apate changamoto mpya.

 Tayari Chelsea wameripotiwa kupeleka dili lao ndani ya Inter Milan ili kupata saini ya kiungo huyo ambaye anatajwa kumvutia Kocha Mkuu wa Chelsea, Thomas Tuchel. 

Ericksen amekuwa na maisha magumu ndani ya Serie A chini ya Kocha Mkuu, Antonio Conte kwa kuwa amekuwa na ushkaji mkubwa na benchi jambo ambalo linatoa nafasi kwa Chelsea kuipata saini yake.

SOMA NA HII  CHELSEA NAO WAANZA MAZUNGUMZO NA HAALAND