Home Ligi Kuu NYOTA WAZAWA WAWILI WAONGEZA AKAUNTI ZA MABAO,TIMU ZAO ZAGAWANA POINTI

NYOTA WAZAWA WAWILI WAONGEZA AKAUNTI ZA MABAO,TIMU ZAO ZAGAWANA POINTI


 NYOTA wa Kagera Sugar, Yusuph Mhilu ameongeza akaunti yake ya mabao kwa kufikisha jumla ya mabao matano kwenye Ligi Kuu Bara sawa na mshakiaji wake Meshack Abraham wa Gwambina FC.

Nyota hao wote wawili waliongeza idadi ya mabao yao wakati walipokutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana, Februari 11, Uwanja wa Kaitaba.

Kagera walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 6 huku Meshack akipachika bao lake la saba dakika ya 90+1 na kuwafanya wagawane jumla ya pointi mbili kwenye mechi mbili ambazo wamekutana.

Kwenye mchezo wa kwanza, Kagera Sugar iliambulia pointi moja ilipokwenda Gwambina Complex kwa sare ya bila kufungana na jana Gwambina nao wakaambulia pointi moja na bao moja.

Mhilu amesema kuwa malengo yao ilikuwa ni kupata pointi tatu ila matokeo yalikuwa tofauti kwao ndani ya dakika 90.

“Tulikuwa tunahitaji pointi tatu ila kwa kuwa wapinzani wetu nao walipambana wakapata bao hakuna namna tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo,” .

Matokeo hayo yanaifanya Kagera Sugar kuwa nafasi ya nane na pointi 23 huku Gwambina FC ikiwa nafasi ya 15 na pointi 20.

SOMA NA HII  WANAUME 22 LEO KAZINI KUSAKA POINTI TATU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here