Home Uncategorized MTAMBO MPYA WA MABAO NDANI YA YANGA WATIMIZA AHADI YA MAMAYE

MTAMBO MPYA WA MABAO NDANI YA YANGA WATIMIZA AHADI YA MAMAYE

 


MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Wazir Junior, amesema anajisikia faraja kupata nafasi ya kucheza Yanga kwani aliweka ahadi kwa mama yake mzazi kabla hajafariki kuwa ipo siku atakuja kuwa mchezaji wa timu hiyo.

 

Wazir amesema mama yake alikuwa na mapenzi makubwa na Yanga enzi za uhai wake, hivyo kutokana na ushabiki huo wa mzazi wake kwa Yanga, akaamua kumpa ahadi kuwa ataongeza juhudi ili siku moja aweze kutua Jangwani.

 

Wazir amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mbao FC, kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaoanza Septemba 6, mwaka huu. Wazir alimaliza msimu akiwa kinara wa mabao ndani ya Mbao akifunga mabao 13. Mama yake mzazi alifariki dunia miaka mitatu iliyopita.

 

Waziri amesema: “Nilimuahidi mama yangu kabla hajafariki ipo siku nitaichezea Yanga. Namshukuru Mwenyezi Mungu nilichomuahidi mama yangu kimetimia, japo yeye hayupo tena kwa sasa ila napata faraja kuona nimetimiza ahadi yake.


“Ndugu zangu pia ni wananchi. Kaka ni Mwanajangwani na mdogo wetu ana mapenzi makubwa na Yanga, hivyo kwao ni furaha baada ya kuona ndugu yao nipo kwenye timu wanayoipenda.”

SOMA NA HII  MUONEKANO wa ukurasa wa mbele wa Gazeti la SPOTI XTRA Alhamisi, lipo mtaani, jipatie nakala yako kwa Tsh 500 tu.